Na Waandishi Wetu
WIKI chache tangu gazeti hili liliporipoti habari iliyohusu
mume wa mtu kunaswa gesti na mwanaume mwenzake, mapema wiki hii, ile
Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ chini ya Global Publishers imenasa
timbwili lingine la aina hiyo gesti.
Tukio
hilo lilishuhudiwa na watu kibao, lilijiri Juni 10, mwaka huu katika
nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Kinondoni jijini Dar.
Kunaswa
kwa wanaume hao ambao ilidaiwa walikuwa kwenye harakati za kufanya
Usodoma na Ugomora, kulifuatia mke wa mmoja wao kunasa meseji za
kimapenzi walizokuwa wakitumiana wawili hao.
Mama huyo alipobaini
meseji hizo chafu, wawili hao wakisisitiziana kukutana kwenye gesti hiyo
usiku wa siku hiyo, alimpigia simu mmoja wa waandishi wa Global ambapo
mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwanamke: Haloo haloo! Nazungumza na mwandishi wa Global?
Mwandishi: Ndiyo, dada tukusaidie nini?
Mwanamke: Naomba msaada wenu jamani, nataka kumfumania mume wangu ana tabia chafu sana!
Mwandishi: Tabia gani?
Mwanamke: Anafanya vitendo vya kishoga na leo amepanga kukutana na huyo
mwanaume mwenzake gesti (akiitaja) iliyopo Kinondoni, nimeona meseji
walizokuwa wakichati.
Mwandishi: Unaweza kuja ofisini kwetu ili tupange namna ya kuwafumania?
Mwanamke: Si hapo Bamaga?
Mwandishi: Naam.
Mwanamke: Kwa kuwa nipo mitaa hii ya Kijitonyama nakuja sasa hivi.
Baada ya nusu saa mama huyo alitinga Makao Makuu ya Global,
Bamaga-Mwenge na kuweka kila kitu wazi ambapo kikosi kazi kilijiandaa
kwa ajili ya kazi hiyo.
FUMANIZI
Ilipofika saa 1:30 usiku, timu yetu, mama huyo, wapambe wake na polisi walikuwa wanafanya doria nje ya gesti hiyo.
WANAUME WATINGA GESTI
Saa 5:30 usiku, mume wa mwanamke huyo akiwa na mwanaume anayedaiwa kuwa
shoga walifika gesti hiyo bila kujua kama waliwekewa mtego wa kunaswa
na kwenda kuchukua chumba namba 2.
Wakiwa ndani, mke alimpigia simu
mumewe na kuhoji alipokuwa akajibiwa alikuwa mitaa ya nyumbani kwao
Manseze, Dar akipiga stori na rafiki zake.
MKE, POLISI, WAANDISHI WATINGA NDANI
Wawili hao wakiwa wanajiandaa na mchezo wao usiofaa, polisi aligonga
mlango akijifanya mhudumu aliyetaka kumpatia taulo, jamaa bila kujua
alifungua ndipo walipofumaniwa na kuibua varangati zito.
Kufuatia
timbwili hilo, waliwekwa chini ya ulinzi na kutolewa pale gesti tayari
kupelekwa kituoni ndipo mwanaume anayedaiwa kuwa shoga akatimbua mbio
mithili ya mwanariadha wa kimataifa, Usain Bolt wa Jamaika na wanandoa
hao waliendelea kuzozana huku mke akimlalamikia mumewe na kumwambia
wakifika nyumbani ampe talaka yake.
Hata hivyo, mwanamke huyo
aliomba sakata hilo lisipelekwe polisi kwa madai alichotaka ni
kumfumania mumewe na kwamba alikuwa na ushahidi wote.
Stori: Kulwa Mwaibale, Issa Mnaly, Richard Bukos.
Source: GlobalPublisher
No comments:
Post a Comment