Biashara zote zilisimama kwa muda katika stendi kuu ya mabasi
ya Bomet nchini kenya wikiendi hii baada ya kundi kubwa la
wanaume kumvamia mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa kingua kifupi
na kisha kumvua huku wengine wakimchezea nyeti zake.....
Mwanamke
huyo ambaye inadaiwa alienda katika stendi hiyo kufanya booking
ya basi,alikutwa na kisanga hicho baada ya kuvamiwa na kundi
kubwa la wapiga debe na vibaka ambao walianza kwa kumzomea na
kumrushia makopo ya maji......
Kwa mujibu wa shuhuda wa
tukio hilo,sakata hilo lilichukua takribani dakika 15 za
kumzomea na kumtukana wakiwa wamemzunguka kabla ya kumvua nguo
zake.....
"Walimzomea na kumtukana vibaya huku wakiwa
wamemzingira.Juhudi za wanawake wasamaria wema kumuokoa zilikwama
kwa kuwa kundi lilikuwa kubwa na wao walikuwa wanaogopa
kufanyiwa hivyo"...Alisema shuhuda huyo
Mbali na shuhuda
huyo,Bwana Sang naye analielezea tukio hilo kwa kudai kuwa ile
sketi ilikuwa ni zaidi ya fupi na pia ilikuwa nyepesi na
ndani ndani hakuwa na kitu, hali iliyosababisha wapiga debe hao
wamvae na kumvua.....
Bwana Sang anadai kuwa kesi nyingi
za ubakaji zimekuwa zikisababishwa na wanawake wenyewe kutokana
na mavazi yao wanayoyavaa....
Baada ya tukio hilo
kupamba moto, polisi walifika japo walichelewa na hatimaye
kufanikiwa kumwokea mrembo huo mikononi mwa vibaka hao....
Kutokana
na tukio hilo,shirika la maendeleo ya wanawake limelaani
vibaya tukio hilo na kuahidi kuchukua hatua kali zaidi endapo
udhalilishaji huo utaendelea na kufumbiwa macho....
SOURCE: udakuspecially.com
No comments:
Post a Comment