Aibu imemshuka, imemfika, imemwenea na imemtapakaa kila upande, Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu.
Hivi leo, endapo utamkuta Wema akiwa ametulia kisha ukamtishia ukitumia
sauti ya juu kuyataja majina ya Diamond na Penny, kuna uwezekano mkubwa
mrembo huyo akavunja mguu kwa kukimbia ‘spidi’ kali.
Ikamshuka
Wema; Jumatatu iliyopita, usiku mkubwa, inadaiwa kuwa mrembo huyo akiwa
katika hali ya utulivu kabisa, akaamua liwalo na liwe, hawezi kulikosa
penzi la mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’, wakati
ni wake tangu na tangu.
Simu ikapigwa; inadaiwa kuwa Wema aliamini Diamond hapindui kwake, kwa hiyo alipiga simu kwa kujiamini.
Kilichozungumzwa; baada ya simu kupokelewa, inadaiwa kwamba Wema aliomba Diamond afungue moyo ili penzi lao lirudi kama zamani. Diamond
kwa misifa; Diamond kwa kiasi fulani alipikwa kimuziki na Dully Sykes
‘Mister Misifa’ na meneja wake wa zamani anaitwa Papa Misifa, kwa hiyo
naye ni zao la Misifa.
Misifa kazini; Diamond aliposikia sauti ya Wema ikimbembeleza, ‘bichwa’ likamvimba, papo hapo, akaanza kumrekodi mrembo huyo. Kilichosikika;
sauti ya Diamond inasikika kwa juu, huku ile ya Wema ikitokelezea kwa
mbali. Kimazungumzo ni kuwa M’bongo Fleva huyo, anaeleza kwamba hivi
sasa yupo kwenye uhusiano ‘siriaz’ na mtangazaji, Penniel Mungilwa
‘Penny’, kwa hiyo hawezi kumwacha.
Eti Diamond hataki ‘drama’;
mwanamuziki huyo, anasikika akimjibu Wema kwamba hawezi kurudiana naye
kwa sababu itaonekana wanafanya drama (maigizo).
Diamond anafunguka:
“Hapa hakuna drama wala nini, wala sikufanyii drama. I am in love with
Penny (nipo kwenye penzi na Penny) na wewe unajua. Sipendi na
sipendezewi kwa sababu mwisho wa siku yatakuja kutokea matatizo,
sitaki.”
Penny naye; mrembo huyo anayemmiliki Diamond kwa sasa,
aliingilia mazungumzo kati ya M’bongo Fleva huyo na Wema, kisha
anasikika akimpa vidonge vyake, mrembo huyo: “Wema unaweza kutuacha
tulale?”
Wema akasalimia; mrembo huyo ambaye juzijuzi alikata
shilingi milioni 13 kumtolea faini msanii Kajala Masanja na kumwokoa na
jela, hakutetereka kusikia sauti ya Penny kwenye simu, badala yake
akamsalimia: “Uko poa?”
Penny akaliendeleza: “Yeah, niko poa mamy
wangu. Hivi kwa nini hutaki kitu kitakachokufanya uwe na amani? Sisi
hatutaki matatizo na wewe.”
WEMA ANASEMAJE?
Alipohojiwa na paparazi wetu kuhusiana na ishu hiyo, Wema alikataa
katakata kwamba sauti inayosikika kwenye rekodi ya mazungumzo hayo siyo
ya kwake, akaongeza kuwa alishaachana na Diamond siku nyingi zilizopita
na kamwe hawezi kufanya kitu kama hicho.
“Hao kama wananichokonoa
wapate ‘kick’ wafanye kimpango wao na siyo kutumia jina langu, mimi ni
staa mkubwa Tanzania na kila mtu ananijua, waniache na maisha yangu kwa
sababu sipendi kuongeaongea. Hata hili kama usingeniuliza, nisingesema
chochote,” alisema mrembo huyo
DIAMOND JE?
Diamond alipozungumza na ripota wetu, alisema kuwa sauti hiyo
alimrekodi Wema kwa lengo la kumwonesha ni kiasi gani hivi sasa yupo
kwenye uhusiano ‘siriaz’ na Penny.
SOURCE: globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment