MWANAMITINDO
‘expensive’ Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ alizidiwa ghafla kwenye
ibada ya kumkumbuka marehemu Steven Kanumba iliyofanyika katika Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Kimara – Temboni, jijini Dar.
Jokate
ambaye awali alikuwa mzima wa afya, alifika kwa ajili ya kujumuika na
familia ya marehemu akiwa na lengo la kukamilisha siku yake kwa kwenda
makaburini na baadaye katika Viwanja vya Leaders kulipokuwa na shughuli
maalum ya kumkumbuka Kanumba lakini alishindwa baada kuzidiwa ghafla.
“Nafikiri alikuwa na uchovu maana anaonekana alikuwa amefanya kazi
nyingi mfululizo kwani alipopelekwa kupumzika ndani ya muda mfupi
alijisikia vizuri,” alisema mmoja wa rafiki wa staa huyo ambaye hakutaka
kutaja jina lake.
SOURCE: globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment