"Shule hii inaitwa Dumanang primary school, ipo katika kijiji
cha lukale wilaya ya Meatu, ambapo kutoka Meatu mjini hadi kijijini hapo ni km
110.
Hii ni shule ambayo inafundisha jamii ya watoto wa Kitaturu.
Shule hii ilifanikiwa kufaulisha watoto saba kati ya kumi
kwenda sekondari ambapo wanne wakiwa wakiume na wakike watatu, lakini kwa
bahati mbaya, watoto watatu walipewa mimba wakiwa sekondari shule za mjini.
Kwa
bahati mbaya mmoja wao alifariki katika harakati za kutoa mamba.
Hii imepelekea jamii ya kitaturu kuomba kuletewa sekondari
karibu na makazi yao,
kufuatia wao kuishi polini, Lakini pia wameomba kuboreshewa shule kutoka kwenye
shule ya miti na kwenda katika shule ya block, ambapo kwa nguvu zao tayari
wamenza maandalizi.
Shule hii kama inavyoonekana hapo juu, madarasa yametenganishwa na miti unayoiona katikati kwa ndani.
Ubao ni mmoja
ambao unafindishiwa darasa la kwanza na kuhamishwa darasa la pili hadi la saba
kwa ubao huo huo mmoja.
Balaa linakuja, pale ambapo mvua ikinyesha hakuna masomo.
Shule ina walimu watatu, wakike wawili na wakiume mmoja, wanafunzi kuanzia darasa la kwanza
hadi la saba wapo 120.
Waheshimiwa naomba kuwasilisha!!"
SOURCE: www.bongoclantz.com
Duuuh! Hii ni hatari! hatari!
ReplyDeleteUtafkiri hawako TZ hii hii dah
ReplyDelete