Thursday, June 13, 2013

Vanessa Ajia Juu, BAB KUBWA

Mtangazaji wa Choice Fm, mwanamuziki, balozi wa vijana Tanzania, ameonyesha kukasirishwa na kitendo cha Gazeti la Babukubwa kuweka picha tofauti na walizokubaliana kwenye ukurasa wa mbele ambao ndio ukurasa wa mauzo wa gazeti (front page)

Akizungumza na XXL vanessa amesema, picha iliyowekwa katika ukurasa wa mbele, sio picha iliyotakiwa kuwepo hapo, walipiga picha nyingi sana wakati wa session ya photo shoot, na kukubaliana picha zinazofaa kutoka lakini matokeo yake wametoa tofauti na makubaliano.

"Tulikuwa tumeshachagua picha za front page na zile zitakazotokea ndani, za front page zilikuwa na version mbili na hakuna hata moja waliyoitoa, hata ukiangalia the headline, Ommy dimpoz ampata Vanessa, ukisoma tu unaelewa nini? ingawa story ni tofauti ndani lakini wangapi wanaliona gazeti na wananua kusoma kilichoandikwa ndani? aliuliza Vanessa. 

"It is so disrespectful, wanaharibu reputation, because my brand doesn't stand for that, wanaweza kukukosesha opportunities in the future."


No comments:

Post a Comment