Vitendo
vya kikatili vimekuwa vikitekelezwa katika sura mbalimbali, ila tukio
la mtumishi wa Mungu, Padri Celestine John Nyaumba, 35, kumgonga kwa
gari makusudi na kumcharanga mapanga mzazi mwenzake ni aibu isiyo na
mfano.
Padri Celestine, anayetoa huduma kwenye Kanisa Katoliki la
Mtakatifu Joseph, Homboro, Dodoma, anatuhumiwa kumtendea unyama huo,
mzazi mwenzake, Selestina Anania Kibena, 35, Jumamosi iliyopita, Kata ya
Kiluvya, Pwani.
Hii ni aibu isiyomithilika kwa sababu padri kufanya
ukatili huo ni kashfa nzito, ongezea kwamba alimfanyia hivyo mzazi
mwenzake, wakati kwa sheria za kanisa, ni mwiko kwa padri kujihusisha na
mapenzi achilia mbali kufikia hatua ya kuzaa.
Aibu hiyo, inapata
uzito zaidi kwa kuwa Selestina (mzazi mwenza wa padri), alikuwa mtawa
(sister), lakini usista ulimshinda baada ya kupata mimba, takriban miaka
minne iliyopita.
Tuesday, April 23, 2013
Thursday, April 18, 2013
Skiliza hapa Bonge moja ya sweet song toka kwa Sayansi
Inasemekana hii Nyimbo ilirekodiwa kabla Q JaY hajaokoka. ni mwimbo mzuri kusema ukweli.
Sayansi Am Sorry ft Q Jay
Ratiba za Series mpaka April 29, 2013
Revolution 2012 S01E14 April 23, 2013
Arrow S01E20 April 25, 2013
Person Of Interest S02E20 April 26, 2013
Nikita S03E18 April 20, 2013
The Good Wife S04E21 April 22, 2013
The Vampire Diaries S04E19 April 19, 2013
Revenge S02E19 April 29, 2013
WEMA ANAMAANISHA ALICHOANDIKA AU NI ANAZINGUA TU?
Kutokana
na kile alaichoandika Wema ameandika hivi “I Pray to God anichukue tu,
nikapumzike, I’m seriously tired…nimechoka mimi” Je anamaanisha au ni
stunt tu ili akick kama alivyosema hakupiga simu kwa Diamond ili
kubembeleza warudiane. Navyomjua Wema sio mtu wa kupaniki kiasi hicho
mpaka aandike vile kwa sababu mwenyewe alishawahi kusema hajali
wanayosema watu na wala hana muda nao, ndo maana ukiangalia ni stunt tu
sidhani kama anamaanisha. Kuna msemo unasema maneno yanaumba,
utakachokisema ndicho kitakacho kutokea kuna mifano mingi sana ukiamua
kufuatilia kuwajua mfano wa haraka ni Tupac na seven days theory
inaonekana ni mtu ambaye alijitabiria kifo chake kwa maneno yake
mwenyewe na wengine unaowajua wewe msomaji.
source: cloudsfm.co
SEKESEKE! MH! MKE AMSHUSHIA KIPIGO MUMEWE BAR
Mwanamke mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, hivi karibuni alizua sekeseke la aina yake baada ya kumvaa mwanaume anayedaiwa ni mume wake na kumshushia kichapo.
WEMA AIBU YAKE! ADAIWA KUPIGIA SIMU DIAMOND NA KUJITONGOZESHA UPYA
Aibu imemshuka, imemfika, imemwenea na imemtapakaa kila upande, Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu.
Hivi leo, endapo utamkuta Wema akiwa ametulia kisha ukamtishia ukitumia sauti ya juu kuyataja majina ya Diamond na Penny, kuna uwezekano mkubwa mrembo huyo akavunja mguu kwa kukimbia ‘spidi’ kali.
Hivi leo, endapo utamkuta Wema akiwa ametulia kisha ukamtishia ukitumia sauti ya juu kuyataja majina ya Diamond na Penny, kuna uwezekano mkubwa mrembo huyo akavunja mguu kwa kukimbia ‘spidi’ kali.
Sunday, April 14, 2013
Friday, April 12, 2013
Hii Picha Nashindwa Elewa ni kwamba shoo ya DIAMOND ilibuma au?
Unaambiwa hii picha imezagaa sana katika mitandao ya kijamii, na inasadikika kwamba ni show ya mchizi DIAMOND. taarifa ni kwamba "Golden Creast Hotel" Mwanza ambapo Diamond alikuwa na show kwaajili ya sikukuu ya wapendanao na kiingilio kinatajwa kuwa kulikuwa
ni shilingi 20,000/- za kitanzania.
Nicki Minaj Na Spika Zake
Wakati wasanii wengine wamekua wakija na Headphones zao Kama Ludacris "Soul By Luda" na 50 "Street King" Mdada minaj ameamua kuja kitofauti kabisa....
Hii ndio biashara mpya ambayo Nicki Minaj ameamua kuanza kuifanya kwa sasa kwa kutengeneza spika ndogo ambazo amezipatia jina Pink Pills ambazo kimsingi watumiaji wake walengwa ni madada duuz... Barbies.

Thursday, April 11, 2013
BREAKING NEWS: DIAMOND AVUNJA RASMI NDOA YA UWOYA
Na Mwandishi Wetu
JAMBO limezua jambo, lile sakata la kunaswa hotelini kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Irene Uwoya limezaa matunda hasi kwa ndoa ya mwadada huyo ambayo sasa imevunjika rasmi, Amani limetonywa.
JAMBO limezua jambo, lile sakata la kunaswa hotelini kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Irene Uwoya limezaa matunda hasi kwa ndoa ya mwadada huyo ambayo sasa imevunjika rasmi, Amani limetonywa.
Wednesday, April 10, 2013
Jokate Azimia Church
MWANAMITINDO
‘expensive’ Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ alizidiwa ghafla kwenye
ibada ya kumkumbuka marehemu Steven Kanumba iliyofanyika katika Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Kimara – Temboni, jijini Dar.
Jokate ambaye awali alikuwa mzima wa afya, alifika kwa ajili ya kujumuika na familia ya marehemu akiwa na lengo la kukamilisha siku yake kwa kwenda makaburini na baadaye katika Viwanja vya Leaders kulipokuwa na shughuli maalum ya kumkumbuka Kanumba lakini alishindwa baada kuzidiwa ghafla.
“Nafikiri alikuwa na uchovu maana anaonekana alikuwa amefanya kazi nyingi mfululizo kwani alipopelekwa kupumzika ndani ya muda mfupi alijisikia vizuri,” alisema mmoja wa rafiki wa staa huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake.
SOURCE: globalpublishers.info

Komesha ya wadada wanaovaa nguo fupi...
Biashara zote zilisimama kwa muda katika stendi kuu ya mabasi
ya Bomet nchini kenya wikiendi hii baada ya kundi kubwa la
wanaume kumvamia mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa kingua kifupi
na kisha kumvua huku wengine wakimchezea nyeti zake.....
Mwanamke huyo ambaye inadaiwa alienda katika stendi hiyo kufanya booking ya basi,alikutwa na kisanga hicho baada ya kuvamiwa na kundi kubwa la wapiga debe na vibaka ambao walianza kwa kumzomea na kumrushia makopo ya maji......
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo,sakata hilo lilichukua takribani dakika 15 za kumzomea na kumtukana wakiwa wamemzunguka kabla ya kumvua nguo zake.....
"Walimzomea na kumtukana vibaya huku wakiwa wamemzingira.Juhudi za wanawake wasamaria wema kumuokoa zilikwama kwa kuwa kundi lilikuwa kubwa na wao walikuwa wanaogopa kufanyiwa hivyo"...Alisema shuhuda huyo
Mbali na shuhuda huyo,Bwana Sang naye analielezea tukio hilo kwa kudai kuwa ile sketi ilikuwa ni zaidi ya fupi na pia ilikuwa nyepesi na ndani ndani hakuwa na kitu, hali iliyosababisha wapiga debe hao wamvae na kumvua.....
Bwana Sang anadai kuwa kesi nyingi za ubakaji zimekuwa zikisababishwa na wanawake wenyewe kutokana na mavazi yao wanayoyavaa....
Baada ya tukio hilo kupamba moto, polisi walifika japo walichelewa na hatimaye kufanikiwa kumwokea mrembo huo mikononi mwa vibaka hao....
Kutokana na tukio hilo,shirika la maendeleo ya wanawake limelaani vibaya tukio hilo na kuahidi kuchukua hatua kali zaidi endapo udhalilishaji huo utaendelea na kufumbiwa macho....
SOURCE: udakuspecially.com

Skendo ya Uwoya + Diamond
Baada ya habari nyingi sana kuhusu Irene Uwoya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Diamond platnumz kutawala vyombo vya habari na kwenye mitandao hapo juzi, hatimaye bongomovies.com tuliamua kumtafuta kwa simu mwanadada Irene Uwoya ili tuweze kumuuliza juu ya tuhuma hizi za yeye kuingilia penzi lwa mwanadada Penny kwa kijana wa “mbongofleva” diamond platnumz.
Baada ya majaribio mengi ya kupiga simu yake ambayo ilikuwa haipatikani muda wote wa mchana baadaye kwenye mida ya saa kumi na mbili hivi jioni tuliweza kumpata hewani na Jibu lake lilikuwa moja tuu kuwa “achana nazo” na sisi tukaona kweli tuachane nazo ila tukufukishie wewe msomaji wetu mpendwa “response” hiyo ili mwenyewe uamue na kutafakari. Hilo ndo jibu alilotupa mwanadada mrembo wa bongo movies Irene Uwoya kuhusu tuhuma za yeye kutoka kimapenzi na msanii Diamond.
Source: www.bongomovies.com
Shule Mkweche Kuliko Zote! Lakini imefaulisha zaidi ya 75% ya Styudentsi wake...
"Shule hii inaitwa Dumanang primary school, ipo katika kijiji
cha lukale wilaya ya Meatu, ambapo kutoka Meatu mjini hadi kijijini hapo ni km
110.
Hii ni shule ambayo inafundisha jamii ya watoto wa Kitaturu.
Shule hii ilifanikiwa kufaulisha watoto saba kati ya kumi
kwenda sekondari ambapo wanne wakiwa wakiume na wakike watatu, lakini kwa
bahati mbaya, watoto watatu walipewa mimba wakiwa sekondari shule za mjini.
Kwa
bahati mbaya mmoja wao alifariki katika harakati za kutoa mamba.
Hii imepelekea jamii ya kitaturu kuomba kuletewa sekondari
karibu na makazi yao,
kufuatia wao kuishi polini, Lakini pia wameomba kuboreshewa shule kutoka kwenye
shule ya miti na kwenda katika shule ya block, ambapo kwa nguvu zao tayari
wamenza maandalizi.
Shule hii kama inavyoonekana hapo juu, madarasa yametenganishwa na miti unayoiona katikati kwa ndani.
Ubao ni mmoja
ambao unafindishiwa darasa la kwanza na kuhamishwa darasa la pili hadi la saba
kwa ubao huo huo mmoja.
Balaa linakuja, pale ambapo mvua ikinyesha hakuna masomo.
Shule ina walimu watatu, wakike wawili na wakiume mmoja, wanafunzi kuanzia darasa la kwanza
hadi la saba wapo 120.
Waheshimiwa naomba kuwasilisha!!"
SOURCE: www.bongoclantz.com
Picha 11 za watoto wa Mastaa wa Bongo
Tuesday, April 9, 2013
Story Za Facebook, Ha ha ha
JAMANI,
HIVI MNAZIJUA GHARAMA ANAZOINGIA BWANA HARUSI HADI ANAPOOA?? ....Katika
hali ya kawaida kabisa, kama wewe ni mwanaume na unataka kuoa, ASEEEE
JIANDAE KWA MAMBO HAYA:
1. Kujitambulisha ukweni. Hapo
utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo mtarajiwa ukajitambulishe
huko. Kama mfano mkeo anatokea "TABORA", na mnaishi Dar, andaa nauli ya
watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharamia shuhuli hiyo ya
utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume mkeo atajitegemea.
Otherwise 800,000 itakutoka.
2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie
nyumbani ni MOSHI utatakiwa umpeleke huko "Uru-Kimanganuni". Sio umlete
hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio kwenu! Andaa nauli yako na
atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na gharama za vinywaji na
chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000
3. Kifuatacho ITV ni
kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane (Ba Mkwe, Ma Mkwe,
Ba Ubatizo, Ma Ubatizo, Mjomba, Shangazi, Kaka mtu na Dada mtu) kutoka
Tabora uwalete Moshi. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We
acha ubishi, tenga 800,000 tu.
4. Kwani we wazazi wako wanajua
unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda TABORA! Watu watano. Utahitaji kuwa
na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna imejensi.
5. MAHARI ndio
topic tatanishi inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye hiyo
safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe
2,000,000.
6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua
ya kawaida kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete
unaweza ita marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe
kabisa. Mi simo
7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi.
Tengeneza kadi za mwaliko wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza
gharama zote ni juu yako. Andaa 500,000. Swali la kwanza kwenye kikao:
“We una shing ngapi?” Sema 1,000,000.
8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu kuna cheka time)
9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa bana!!
10. “Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?” 300,000!
11. “Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send…” 400,000!
12. “Baby, rafiki yangu Maimartha alinunua gauni la harusi China yani lilimpendezajee” 700,000!
13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za
harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000
maana utalia lia sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala
hutarudishiwa.
14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda
mwenyewe? Ndugu wawili watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off
utatakiwa kutoa sijui blanketi la bibi, vitenge vya mashangazi, na
vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000 uende navyo ili kupunguza
gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi watakaoibuka ghafla!
15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.
16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000
17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.
18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa
uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji kama 500,000
19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000
20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa wakapambwe saluni. 200,000
21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele na black kibishi 40,000
22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana
akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo,
so utalipa malazi ya siku mbili 200,000
23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini ya 800,000 kwa angalau siku 3.
24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae
hakuchanga anakupigia simu “Mangi eeeeh, Sasa tunavunja lini kamati?”
Pesa yote iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja
kamati ni za nani?? 500,000!
25. SASA MNAANZA MAISHA YA UNYUMBA.
14,180,000 poorer.ASEEEEEE, YAANI UKIYAFIKIRIA HAYA, NDO YANAPOKUJA YALE
YA "Brey Ehhh, we yako lini bana???" NAYE ANAWAJIBU "Aseee, mi bado
nipo nipo kwanza"!!
Picha 6 na Habari kuhusu Wabunge walionenda Jeshini
Kutoka Kushoto Mh. Halima Mdee, Esther Bulaya na Neema Hamaid |
Kuonesha jinsi ambavyo msoto ulikuwa wa nguvu, katika kambi ya Tanga, siku tu ya utambulisho, mbunge wa Chadema (jina tunalo), alizimia.
Vilevile, kwenye Kambi namba 832, Ruvu, Pwani, Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine, alishindwa kuhimili kishindo cha depo, hivyo akatoroka, japo mafunzo yenyewe yalikuwa ya muda wa wiki tatu tu
Mh Mdee akinyolewa |
Unaambiwa Siku ya kwanza tu ya kuripoti kambini, wabunge wote walipigwa vipara na baada ya hapo, ilifuata awamu ya kupima afya.
“Jeshi ni jeshi tu, tulipimwa ukimwi bila hata kuandaliwa wala kupewa ushauri,” alisema mmoja wa wabunge waliohudhuria depo hiyo (jina tunalo) kisha akaongeza: “Mfano mimi ningeambiwa kule kuna kupima ukimwi hata nisingeenda, nilikuwa sijapima kama miaka saba, dah kule ni hatari.”
Picha ya Wabunge na wanajeshi |
“Tatizo unanyolewa halafu ndiyo unapelekwa kupimwa ukimwi, sasa ukikataa kupima na una kipara chako, mtaani utarudi vipi? Hata kunyoa, wengine tuliingia na rasta, lakini wakatupiga upara wa wembe harakaharaka bila hata kungoja kuzifumua.”
Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Umoja wa Vijana wa CCM, Mkoa wa Mara, Ester Bulaya, alisema kuwa anashukuru kupata mafunzo ya kijeshi, kwani yamemjenga kwa kiasi kikubwa.
“Japo ni kazi lakini tunatamani muda uongezwe, maana wiki tatu zilikuwa fupi, program ni nyingi, kwa hiyo tukatakiwa kufanya kwa pamoja,” alisema Bulaya kisha akaongeza: “Imenijenga kweli, najiona mkakamavu mwenye uwezo zaidi wa kutumikia wananchi.”
Kwa upande wa Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, alisema: “Natamani kila mtu awe anapitia mafunzo ya JKT, maana siyo tu yanakujenga kiukakamavu, bali pia yanakupa uzalendo na ari ya kuwatumikia wananchi.”
PICHA NA HABARI ZOTE KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHER.
Serikali Kurudisha Adhabu ya Viboko kwa wanafunzi ili kujenga Nidhamu
Serikali imesema itarudisha adhabu ya viboko kwa wanafunzi
shuleni ili kujenga nidhamu na kujituma.Akizungumza Dar es Salaam jana
wakati akizindua tovuti ya www.shuledirect.co.tz inayowezesha wanafunzi
kujisomea kwa njia ya mtandao, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Philipo Mulugo ilisema kuondolewa kwa adhabu ya viboko shuleni
kumewafanya wanafunzi wengi kukosa nidhamu na wakati mwingine kujifanyia
mambo kienyeji.
“Wasipotandikwa mambo hayaendi, nilipokuwa mwalimu mkuu nilikuwa nawatandika kweli ndiyo maana shule yangu ilikuwa ikiongoza Mkoa wa Mbeya hivihivi hawaendi...” alisema huku akishangiliwa na wageni waalikwa.
Alisema watoto wa siku hizi wamekuwa wakitumia vibaya teknolojia ambayo ingeweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika masomo yao... “Tovuti kama hiyo ingewasaidia kwa masomo, lakini wao wanakimbilia kwenye facebook na mambo mengine yasiyofaa.”
Aliyalaumu mashirika yasiyo ya kiserikali na haki za binadamu ambayo yamekuwa yakipigania kuondolewa kwa adhabu hiyo shuleni na kusababisha kushuka kwa nidhamu kwa kiasi kikubwa.
Kadhalika alisema Serikali imepiga marufuku matumizi ya simu za mikononi kwa sababu baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakizitumia vibaya jambo ambalo linawarudisha nyuma kimasomo.
“Simu tunazipiga marufuku, mwalimu akimkuta mwanafunzi na simu amnyang’anye ndizo zinatuharibia taifa letu.”
Aliwapongeza wabunifu wa mtandao huo akisema ni wazalendo kwani wamekuwa msaada katika jitihada za Serikali kukuza elimu nchini.

Baadhi ya Series pamoja na release dates zake mpaka April 29, 2013
Revolution 2012 S01E12 April 2, 2013
Arrow S01E19 April 4, 2013
Person Of Interest S02E19 April 5, 2013
Nikita S03E16 April 6, 2013
The Good Wife S04E20 April 15, 2013
The Vampire Diaries S04E19 April 19, 2013
Revenge S02E19 April 29, 2013
Bow Wow Ashtakiwa na mdada mcheza picha za Ngono
Memba wa kundi la YMCMB ambae pia ni mtangazaji wa kipindi cha 106 N Park ya huko marekani, amejikuta matatani baada ya kushtakiwa na mdada mcheza picha za Ngono, maarufu kama 'Katsuni'. Ambae inaaminika kuwa Bow wow ametumia moja ya 'Dance style' za huyo dada bila kupata kibali toka kwa huyo mdada, hivyo sasa jamaa ana 'face' msala. Na inakadiriwa endapo huyo dada atashinda hiyo kesi basi itamlazimu Bow wow amlipe $80,000 ambazo kwa hela za kibongo ni kama 129,479,170.04 tshs kitu kama milion mia ishirini na tisa laki nne na vimchuzi mchuzi huko... Duh!
Subscribe to:
Posts (Atom)