Monday, June 17, 2013

KURUDIANA KATI YA AMINI NA LIHAH,AMIN ALIONGOPA AMA WAMEPIGANA CHINI TENA.?


Week chache zilizopita mtu mzima Amin aliongea exclusive  teentz na kusema kuwa yeye na dada etu Linah wameludiana kimapenzi,ingawa side B kwa upande wa Linah hakusema chochote kuhusu ishu hiyo
kupitia instagram Fineassgirl aka Masogange amepost picha ya Linah na Mshikaji anayemwita kaka .picha na maelezo vikionyesha hawa wawili tayari wana mchezo wa i love you,i love you too
 …

So amin aliongopa ama wameachana tena???
............................NOMA SANA..........

Source: TeenTz

Saturday, June 15, 2013

Mtu wa Nguvu ashambuliwa na watu wake Wa Nguvu

 Katika hali isiyo kawaida jana Mtu wa Nguvu alipost
status facebook iliyokua na link zenye picha ya Show ya Mwana Fa, Baada ya tukio ndipo watu wa nguvu wakaanza mshambulia kwa maneno, wengine wakimpa ushauri, na wengine hata matusi pia.. ila cheki mwenyewe hizo comments katika hiyo post, zingine nimeshindwa kuziweka maana zina matusi mazito nikaona si vyema kuyaweka hapa..

Thursday, June 13, 2013

Baadhi ya Tweets za wasanii walioshtushwa na Kifo cha Langa


Mke amfumania Mumewe akifanya vitendo vya ushoga!

Na Waandishi Wetu
WIKI chache tangu gazeti hili liliporipoti habari iliyohusu mume wa mtu kunaswa gesti na mwanaume mwenzake, mapema wiki hii, ile Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ chini ya Global Publishers imenasa timbwili lingine la aina hiyo gesti.

Vanessa Ajia Juu, BAB KUBWA

Mtangazaji wa Choice Fm, mwanamuziki, balozi wa vijana Tanzania, ameonyesha kukasirishwa na kitendo cha Gazeti la Babukubwa kuweka picha tofauti na walizokubaliana kwenye ukurasa wa mbele ambao ndio ukurasa wa mauzo wa gazeti (front page)

Lady Jay Dee Poster


Tuesday, April 23, 2013

Padre amkata amkata Mapanga Mwanamke Aliyezaa naye mtoto duh!

Vitendo vya kikatili vimekuwa vikitekelezwa katika sura mbalimbali, ila tukio la mtumishi wa Mungu, Padri Celestine John Nyaumba, 35, kumgonga kwa gari makusudi na kumcharanga mapanga mzazi mwenzake ni aibu isiyo na mfano.
Padri Celestine, anayetoa huduma kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Homboro, Dodoma, anatuhumiwa kumtendea unyama huo, mzazi mwenzake, Selestina Anania Kibena, 35, Jumamosi iliyopita, Kata ya Kiluvya, Pwani.
Hii ni aibu isiyomithilika kwa sababu padri kufanya ukatili huo ni kashfa nzito, ongezea kwamba alimfanyia hivyo mzazi mwenzake, wakati kwa sheria za kanisa, ni mwiko kwa padri kujihusisha na mapenzi achilia mbali kufikia hatua ya kuzaa.
Aibu hiyo, inapata uzito zaidi kwa kuwa Selestina (mzazi mwenza wa padri), alikuwa mtawa (sister), lakini usista ulimshinda baada ya kupata mimba, takriban miaka minne iliyopita.

Thursday, April 18, 2013

Enjoy....


Nyimbo Ya kumuenzi Bi Kidude By Peter Msechu

Peter Msechu Lala Bi. Kidude

Skiliza hapa Bonge moja ya sweet song toka kwa Sayansi

Inasemekana hii Nyimbo ilirekodiwa kabla Q JaY hajaokoka. ni mwimbo mzuri kusema ukweli. Sayansi Am Sorry ft Q Jay

Ratiba za Series mpaka April 29, 2013

Revolution 2012 S01E14 April 23, 2013

Arrow S01E20 April 25, 2013

Person Of Interest S02E20 April 26, 2013

Nikita S03E18 April 20, 2013

The Good Wife S04E21 April 22, 2013

The Vampire Diaries S04E19 April 19, 2013

Revenge S02E19 April 29, 2013

WEMA ANAMAANISHA ALICHOANDIKA AU NI ANAZINGUA TU?



Kutokana na kile alaichoandika Wema ameandika hivi “I Pray to God anichukue tu, nikapumzike, I’m seriously tired…nimechoka mimi” Je anamaanisha au ni stunt tu ili akick kama alivyosema hakupiga simu kwa Diamond ili kubembeleza warudiane. Navyomjua Wema sio mtu wa kupaniki kiasi hicho mpaka aandike vile kwa sababu mwenyewe alishawahi kusema hajali wanayosema watu na wala hana muda nao, ndo maana ukiangalia ni stunt tu sidhani kama anamaanisha. Kuna msemo unasema maneno yanaumba, utakachokisema ndicho kitakacho kutokea kuna mifano mingi sana ukiamua kufuatilia kuwajua mfano wa haraka ni Tupac na seven days theory inaonekana ni mtu ambaye alijitabiria kifo chake kwa maneno yake mwenyewe na wengine unaowajua wewe msomaji.
Kwa maneno kama hayo mtu anayeweza kusema ni mtu Yule ambaye ameshindwa maisha hana kitu kabisa ni maskini ambaye hata mlo mmoja kwa siku ni shida au mtu ambae ni mgonjwa ambae hana matumaini kabisa ya kupona na ameumwa kwa siku, lakini sio Wema mtu maarufu mwenye utajiri wa kutosha akiwa na umri mdogo huku akiwa na mipango mingi kwa baadae. Kwa hiyo naona hizo ni stunt tu pia Wema akiwa anataka aendelee kuckick zaidi.
 
source: cloudsfm.co

Listen to Stella Mwangi ft Mahombi Hula Hoop

SEKESEKE! MH! MKE AMSHUSHIA KIPIGO MUMEWE BAR

Stori:Mwandishi Wetu
Mwanamke mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, hivi karibuni alizua sekeseke la aina yake baada ya kumvaa mwanaume anayedaiwa ni mume wake na kumshushia kichapo.
Tukio hilo la aina yake lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Baa ya Corner iliyopo Afrikasana, Sinza jijini Dar ambapo inadaiwa chanzo cha vurumai hilo ni mwanaume huyo kutoonekana nyumbani.

WEMA AIBU YAKE! ADAIWA KUPIGIA SIMU DIAMOND NA KUJITONGOZESHA UPYA

 Aibu imemshuka, imemfika, imemwenea na imemtapakaa kila upande, Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu.

Hivi leo, endapo utamkuta Wema akiwa ametulia kisha ukamtishia ukitumia sauti ya juu kuyataja majina ya Diamond na Penny, kuna uwezekano mkubwa mrembo huyo akavunja mguu kwa kukimbia ‘spidi’ kali.

Friday, April 12, 2013

Hii Picha Nashindwa Elewa ni kwamba shoo ya DIAMOND ilibuma au?

Unaambiwa hii picha imezagaa sana katika mitandao ya kijamii, na inasadikika kwamba ni show ya mchizi DIAMOND. taarifa ni kwamba "Golden Creast Hotel" Mwanza ambapo Diamond alikuwa na show kwaajili ya sikukuu ya wapendanao na kiingilio kinatajwa kuwa kulikuwa ni shilingi 20,000/- za kitanzania.

Nicki Minaj Na Spika Zake

Wakati wasanii wengine wamekua wakija na Headphones zao Kama Ludacris "Soul By Luda" na 50 "Street King" Mdada minaj ameamua kuja kitofauti kabisa....

 Hii ndio biashara mpya ambayo Nicki Minaj ameamua kuanza kuifanya kwa sasa kwa kutengeneza spika ndogo ambazo amezipatia jina Pink Pills ambazo kimsingi watumiaji wake walengwa ni madada duuz... Barbies.

Ngoma Mpya Ya Diamond Iskilize Hapa


 Mapenzi Basi - Diamond

Thursday, April 11, 2013

BREAKING NEWS: DIAMOND AVUNJA RASMI NDOA YA UWOYA

Na Mwandishi Wetu
JAMBO limezua jambo, lile sakata la kunaswa hotelini kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Irene Uwoya limezaa matunda hasi kwa ndoa ya mwadada huyo ambayo sasa imevunjika rasmi, Amani limetonywa.

Eti Unaambiwa hii ndo Kawe Mpya itakayokuja.


Wednesday, April 10, 2013

Jokate Azimia Church

 MWANAMITINDO ‘expensive’ Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ alizidiwa ghafla kwenye ibada ya kumkumbuka marehemu Steven Kanumba iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Kimara – Temboni, jijini Dar.
Jokate ambaye awali alikuwa mzima wa afya, alifika kwa ajili ya kujumuika na familia ya marehemu akiwa na lengo la kukamilisha siku yake kwa kwenda makaburini na baadaye katika Viwanja vya Leaders kulipokuwa na shughuli maalum ya kumkumbuka Kanumba lakini alishindwa baada kuzidiwa ghafla.
“Nafikiri alikuwa na uchovu maana anaonekana alikuwa amefanya kazi nyingi mfululizo kwani alipopelekwa kupumzika ndani ya muda mfupi alijisikia vizuri,” alisema mmoja wa rafiki wa staa huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake.

SOURCE: globalpublishers.info

Komesha ya wadada wanaovaa nguo fupi...

Biashara  zote  zilisimama  kwa  muda  katika  stendi  kuu ya mabasi  ya  Bomet  nchini  kenya wikiendi  hii  baada  ya  kundi  kubwa  la  wanaume  kumvamia  mwanamke  mmoja  aliyekuwa  amevaa  kingua  kifupi  na  kisha  kumvua  huku  wengine  wakimchezea  nyeti  zake.....

Mwanamke  huyo ambaye inadaiwa  alienda  katika  stendi  hiyo  kufanya  booking  ya  basi,alikutwa  na  kisanga  hicho  baada  ya  kuvamiwa  na  kundi  kubwa  la  wapiga  debe  na  vibaka  ambao  walianza  kwa  kumzomea  na  kumrushia  makopo  ya  maji......

Kwa  mujibu  wa  shuhuda  wa  tukio  hilo,sakata  hilo  lilichukua  takribani  dakika  15  za  kumzomea  na  kumtukana  wakiwa  wamemzunguka  kabla  ya  kumvua  nguo  zake.....

"Walimzomea  na  kumtukana  vibaya  huku  wakiwa  wamemzingira.Juhudi za  wanawake  wasamaria  wema  kumuokoa  zilikwama  kwa  kuwa  kundi  lilikuwa  kubwa  na  wao  walikuwa  wanaogopa  kufanyiwa  hivyo"...Alisema  shuhuda  huyo

Mbali  na  shuhuda  huyo,Bwana  Sang  naye  analielezea  tukio  hilo  kwa  kudai  kuwa  ile  sketi  ilikuwa  ni  zaidi  ya  fupi  na  pia  ilikuwa nyepesi  na  ndani  ndani  hakuwa  na  kitu, hali  iliyosababisha  wapiga  debe  hao  wamvae  na  kumvua.....

Bwana  Sang  anadai  kuwa  kesi  nyingi  za  ubakaji  zimekuwa  zikisababishwa  na  wanawake  wenyewe  kutokana  na  mavazi  yao  wanayoyavaa....

Baada  ya  tukio  hilo  kupamba  moto, polisi  walifika  japo  walichelewa  na  hatimaye  kufanikiwa  kumwokea  mrembo  huo  mikononi  mwa  vibaka  hao....

Kutokana  na  tukio  hilo,shirika  la  maendeleo  ya  wanawake  limelaani  vibaya  tukio  hilo  na  kuahidi  kuchukua  hatua  kali  zaidi  endapo  udhalilishaji  huo  utaendelea  na  kufumbiwa  macho....
SOURCE: udakuspecially.com

Skendo ya Uwoya + Diamond


Baada ya habari nyingi sana kuhusu Irene Uwoya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Diamond platnumz kutawala vyombo vya habari na kwenye mitandao hapo juzi, hatimaye bongomovies.com tuliamua kumtafuta kwa simu mwanadada Irene Uwoya ili tuweze kumuuliza juu ya tuhuma hizi za yeye kuingilia penzi lwa mwanadada Penny kwa kijana wa “mbongofleva” diamond platnumz.
Baada ya majaribio mengi ya kupiga simu yake ambayo ilikuwa haipatikani muda wote wa mchana baadaye kwenye mida ya saa kumi na mbili hivi jioni tuliweza kumpata hewani na Jibu lake lilikuwa moja tuu kuwa “achana nazo” na sisi tukaona kweli tuachane nazo ila tukufukishie wewe msomaji wetu mpendwa “response” hiyo ili mwenyewe uamue na kutafakari. Hilo ndo jibu alilotupa mwanadada mrembo wa bongo movies Irene Uwoya kuhusu tuhuma za yeye kutoka kimapenzi na msanii Diamond.

Source: www.bongomovies.com

Shule Mkweche Kuliko Zote! Lakini imefaulisha zaidi ya 75% ya Styudentsi wake...




"Shule hii inaitwa Dumanang primary school, ipo katika kijiji cha lukale wilaya ya Meatu, ambapo kutoka Meatu mjini hadi kijijini hapo ni km 110.
Hii ni shule ambayo inafundisha jamii ya watoto wa Kitaturu.
Shule hii ilifanikiwa kufaulisha watoto saba kati ya kumi kwenda sekondari ambapo wanne wakiwa wakiume na wakike watatu, lakini kwa bahati mbaya, watoto watatu walipewa mimba wakiwa sekondari shule za mjini.
Kwa bahati mbaya mmoja wao alifariki katika harakati za kutoa mamba.
Hii imepelekea jamii ya kitaturu kuomba kuletewa sekondari karibu na makazi yao, kufuatia wao kuishi polini, Lakini pia wameomba kuboreshewa shule kutoka kwenye shule ya miti na kwenda katika shule ya block, ambapo kwa nguvu zao tayari wamenza maandalizi.
Shule hii kama inavyoonekana hapo juu,  madarasa yametenganishwa na miti unayoiona katikati kwa ndani. 
Ubao ni mmoja ambao unafindishiwa darasa la kwanza na kuhamishwa darasa la pili hadi la saba kwa ubao huo huo mmoja.
Balaa linakuja, pale ambapo mvua ikinyesha hakuna masomo.
Shule ina walimu watatu, wakike wawili na wakiume mmoja, wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba wapo 120.
Waheshimiwa naomba kuwasilisha!!"

Picha 11 za watoto wa Mastaa wa Bongo


mtoto wa Allan Lucky: Brooklyn


Mtoto wa Madee: Sophy



Mtoto wa Mwana FA: Malaika

Michelle wa Mike T

Queen na Baba ake Gelly wa Rhymes

Barnaba Product: Steve

Shilole Product: Joyce



Source: Annapita/ Irene Mwamfupe Jamii









Tuesday, April 9, 2013

Story Za Facebook, Ha ha ha

JAMANI, HIVI MNAZIJUA GHARAMA ANAZOINGIA BWANA HARUSI HADI ANAPOOA?? ....Katika hali ya kawaida kabisa, kama wewe ni mwanaume na unataka kuoa, ASEEEE JIANDAE KWA MAMBO HAYA:

1. Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo mtarajiwa ukajitambulishe huko. Kama mfano mkeo anatokea "TABORA", na mnaishi Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharamia shuhuli hiyo ya utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume mkeo atajitegemea. Otherwise 800,000 itakutoka.
2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni MOSHI utatakiwa umpeleke huko "Uru-Kimanganuni". Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na gharama za vinywaji na chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000

3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane (Ba Mkwe, Ma Mkwe, Ba Ubatizo, Ma Ubatizo, Mjomba, Shangazi, Kaka mtu na Dada mtu) kutoka Tabora uwalete Moshi. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha ubishi, tenga 800,000 tu.
4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda TABORA! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna imejensi.

5. MAHARI ndio topic tatanishi inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe 2,000,000.
6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo

7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa 500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: “We una shing ngapi?” Sema 1,000,000.
8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu kuna cheka time)

9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa bana!!
10. “Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?” 300,000!
11. “Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send…” 400,000!
12. “Baby, rafiki yangu Maimartha alinunua gauni la harusi China yani lilimpendezajee” 700,000!

13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000 maana utalia lia sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala hutarudishiwa.
14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000 uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi watakaoibuka ghafla!

15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.
16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000
17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.

18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji kama 500,000
19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000

20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa wakapambwe saluni. 200,000
21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele na black kibishi 40,000
22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so utalipa malazi ya siku mbili 200,000
23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini ya 800,000 kwa angalau siku 3.

24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae hakuchanga anakupigia simu “Mangi eeeeh, Sasa tunavunja lini kamati?” Pesa yote iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za nani?? 500,000!
25. SASA MNAANZA MAISHA YA UNYUMBA. 14,180,000 poorer.ASEEEEEE, YAANI UKIYAFIKIRIA HAYA, NDO YANAPOKUJA YALE YA "Brey Ehhh, we yako lini bana???" NAYE ANAWAJIBU "Aseee, mi bado nipo nipo kwanza"!!

Picha 5 za Nicki Minaj Kabla hajajifanyia Upasuaji & Na baada ya kufanya upasuaji

...Unaona Mwenyewe...



Enzi hizoooo

Kabla hajaongeza kalio na baada



hii wakati yuko High School

Picha 6 na Habari kuhusu Wabunge walionenda Jeshini

Kutoka Kushoto Mh. Halima Mdee, Esther Bulaya na Neema Hamaid
WABUNGE katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao walihudhuria mafunzo ya kijeshi katika kambi tofauti za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), walipata msoto wa nguvu. Tofauti na ilivyokuwa ikidhaniwa kwamba wabunge hao wangepewa mafunzo kwa kubembelezwa kutokana na nafasi zao, walikutana na msoto wa nguvu mwanzo hadi mwisho.
Kuonesha jinsi ambavyo msoto ulikuwa wa nguvu, katika kambi ya Tanga, siku tu ya utambulisho, mbunge wa Chadema (jina tunalo), alizimia.
Vilevile, kwenye Kambi namba 832, Ruvu, Pwani, Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine, alishindwa kuhimili kishindo cha depo, hivyo akatoroka, japo mafunzo yenyewe yalikuwa ya muda wa wiki tatu tu

Mh Mdee akinyolewa

Unaambiwa Siku ya kwanza tu ya kuripoti kambini, wabunge wote walipigwa vipara na baada ya hapo, ilifuata awamu ya kupima afya.
“Jeshi ni jeshi tu, tulipimwa ukimwi bila hata kuandaliwa wala kupewa ushauri,” alisema mmoja wa wabunge waliohudhuria depo hiyo (jina tunalo) kisha akaongeza: “Mfano mimi ningeambiwa kule kuna kupima ukimwi hata nisingeenda, nilikuwa sijapima kama miaka saba, dah kule ni hatari.”
Picha ya Wabunge na wanajeshi
 Mbunge mwingine alisema: “Walichotuweza ni ile tunaripoti tu, tunanyolewa vipara halafu ndiyo taratibu nyingine zinafuata. Kama wangekuwa wanatuonesha picha ya kile kitakachofanyika kabla ya kutunyoa, wengi wetu tungetimka mapema.
“Tatizo unanyolewa halafu ndiyo unapelekwa kupimwa ukimwi, sasa ukikataa kupima na una kipara chako, mtaani utarudi vipi? Hata kunyoa, wengine tuliingia na rasta, lakini wakatupiga upara wa wembe harakaharaka bila hata kungoja kuzifumua.”

Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Umoja wa Vijana wa CCM, Mkoa wa Mara, Ester Bulaya, alisema kuwa anashukuru kupata mafunzo ya kijeshi, kwani yamemjenga kwa kiasi kikubwa.
“Japo ni kazi lakini tunatamani muda uongezwe, maana wiki tatu zilikuwa fupi, program ni nyingi, kwa hiyo tukatakiwa kufanya kwa pamoja,” alisema Bulaya kisha akaongeza: “Imenijenga kweli, najiona mkakamavu mwenye uwezo zaidi wa kutumikia wananchi.”
Kwa upande wa Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, alisema: “Natamani kila mtu awe anapitia mafunzo ya JKT, maana siyo tu yanakujenga kiukakamavu, bali pia yanakupa uzalendo na ari ya kuwatumikia wananchi.”


PICHA NA HABARI ZOTE KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHER.